BENKI YA CRDB YAFADHILI UJENZI WA KLINIKI YA MAT SHINYANGA, DCEA YAHIMIZA USHIRIKIANO WA JAMII


Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo (wa pili kushoto), akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yudas Ndungile, wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akifuatiwa na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia. 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment - MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.

***

Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog

Benki ya CRDB imetoa ufadhili wa shilingi milioni 145 kwa Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kujenga Kliniki mpya ya Tiba ya MAT (Medically-Assisted Treatment) katika Manispaa ya Shinyanga, hatua ambayo inaimarisha juhudi za Serikali za kupambana na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Kliniki hiyo imejengwa kwa ushirikiano wa THPS, Benki ya CRDB, Wizara ya Afya, DCEA, na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, ikizingatia viwango vya kitaifa vya huduma za afya.

Kituo hicho kimekabidhiwa rasmi na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, katika hafla iliyofanyika Jumapili, Machi 22, 2026.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kamishna Lyimo amelipongeza Shirika la THPS na CRDB Bank kwa mchango wao mkubwa, akisema: “Naipongeza THPS kwa jitihada zao za kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Pia naishukuru Benki ya CRDB kwa msaada wao mkubwa. Nawahimiza wananchi, hususan vijana walioathirika, kutumia huduma hizi ili kwa pamoja tulinde afya na mustakabali wa jamii zetu.”

Lyimo ametoa wito kwa taasisi nyingine za fedha na sekta binafsi kuiga mfano wa CRDB kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto za kijamii, akibainisha kuwa mchango huo umeokoa rasilimali za Serikali na kuboresha moja kwa moja huduma za afya kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia, amesema kliniki hiyo ni ya kwanza katika Mkoa wa Shinyanga na kabla ya kuanzishwa kwake, waraibu wengi walilazimika kusafiri hadi Mwanza kupata matibabu. 

“Naishukuru Benki ya CRDB kwa ufadhili huu na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake. Huu ni mfano mzuri wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika kuimarisha upatikanaji, usawa na ubora wa huduma za afya”, ameongeza Dkt. Redempta.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid M. Nsekela, amesema benki hiyo ina utaratibu wa kutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi (VAT) kwa ajili ya kurejesha kwa jamii kupitia miradi ya afya, elimu, mazingira na maeneo mengine ya kijamii.

“Benki ya CRDB inathamini ushirikiano wake na THPS pamoja na Serikali ya Tanzania na zaidi niwapongeza THPS ambao walileta kwetu wazo hili na sisi tukafanya ufadhili huu. Kusaidia ujenzi wa kliniki hii ni kielelezo cha dhamira yetu ya kuboresha ustawi wa jamii tunamofanya biashara na kuifanya benki ya CRDB kuwekeza kwa jamii badala ya kufanya biashara pekee. Tukiwa kama benki kiongozi nchini Tanzania, tutaendelea kuunga mkono programu zenye matokeo chanya na endelevu kwa jamii,” amesema Wagana.

“Huu ni mwendelezo na tunaahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kusaidia miradi ya serikali. Tunaamini katika mashirikiano ya Serikali na sekta binafsi ndo chachu ya mafanikio katika maendeleo. Mwisho tunawaomba wadau wote – wafanyakazi, wafanyabiashara, wastaafu, vijana, na makundi yote – kuendelea kutumia huduma za CRDB nchini Tanzania ili asilimia moja baada ya kodi iweze kuongezeka na kusaidia maeneo mbalimbali yenye uhitaji”,ameongeza Wagana.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, amesema maandalizi ya kliniki yamekamilika, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa watumishi wa afya, samani na maboresho ya mazingira, ili kuhakikisha huduma zinaanza kutolewa kwa ufanisi. 

Pia ameomba wadau kuendelea kusaidia kliniki hiyo kwa vifaa muhimu kama mashine za kupima kiwango cha matumizi ya dawa ili kusaidia kupanga dozi sahihi kwa wagonjwa.
Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo (wa pili kushoto), akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya  MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, pamoja na Mkurugenzi wa Tanzania Health Promotion Support, Redempta Mbatia. 
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia (wa pili kulia) akizungumza wakati Uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, akifuatiwa na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia (wa pili kulia) akizungumza wakati Uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kliniki ya MAT iliyojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akifuatiwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi. Wa kwanza kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, pamoja na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akipata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa katika Kliniki ya MAT kutoka kwa mtaalamu wa afya.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (katikati), akipata maelezo kuhusu Huduma zinazotolewa katika Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati akitembelea Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akielezea kuhusu Huduma zinazotolewa katika Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment - MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kuhusu umuhimu wa huduma za MAT katika kupambana na uraibu wa dawa za kulevya.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John akielezea namna huduma zitakavyotolewa.
Kamishna wa Kinga na Tiba wa DCEA, Dkt. Peter Patrick Mfisi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mnufaika wa huduma za MAT, Ibrahim Seif akieleza jinsi alivyofanikiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya baada ya miaka 10.
Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Kamishna wa Kinga na Tiba wa DCEA, Dkt. Peter Patrick Mfisi
Picha ya pamoja Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo , viongozi mbalimbali pamoja na maafisa wa Benki ya CRDB.
Picha ya pamoja ya Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, viongozi mbalimbali na wanufaika wa huduma za MAT.
Picha ya pamoja Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo , viongozi mbalimbali pamoja na maafisa wa Benki ya CRDB na THPS.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post