MADIWANI KISHAPU WAPITISHA BAJETI YA BILION 54.3 MWAKA WA FEDHA 2026/2027

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani humo cha kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 54.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Februari 12,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo

Na Ofisi ya Habari Kishapu

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga  limeidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 54.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 2.8 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.


Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, kwenye kikao kilichofanyika Februari 12, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Josephat Limbe, amewapongeza madiwani kwa kujadili kwa kina randama ya bajeti kuanzia ngazi ya kamati za kudumu hadi vikao vya vyama vya siasa kabla ya kuidhinishwa rasmi na baraza.


Amesisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa mapato ya ndani ili kuhakikisha utekelezaji wa mipango yote iliyopangwa.


“Nawasihi Waheshimiwa Madiwani kushiriki kikamilifu katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ndani ya kata zenu ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli zote za halmashauri na miradi ya maendeleo,” ameongeza Limbe.


Kwa upande wake, Muwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa alisisitiza umuhimu wa nidhamu katika usimamizi wa mapato, akieleza kuwa mafanikio ya bajeti hiyo yanategemea ukusanyaji na matumizi sahihi ya fedha.Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shiyanga Mhe. Enock R. Bundala akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani humo cha kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 54.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Februari 12,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo


“Tusiposimamia usimamizi wa mapato haya, yote tunayoyaomba hayatatimia,” ameeleza.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohammed, amewapongeza madiwani kwa kupitisha bajeti hiyo na kushauri Halmashauri kuendelea kubuni na kuimarisha vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza uwezo wa kifedha wa Wilaya.


Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya  Emmanuel Johnson, amewapongeza wataalamu wa halmashauri kwa kuandaa bajeti hiyo kwa weledi. Aidha, amewataka madiwani kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii ikiwemo kuhamasisha uandikishaji wa watoto wa shule ya awali na kidato cha kwanza, pamoja na uhamasishaji wa Bima ya afya kwa wote na utambuzi wa Kaya zisizo na uwezo ili ziweze kunufaika na mpango wa kugharamiwa na Serikali.


Katika kikao hicho, Meneja wa TARURA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Elia Mgaya, amewasilisha mpango wa bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 huku Madiwani wakiweka azimio la kuomba fedha kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara, wakieleza kuwa barabara bora ni msingi wa kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika wilaya hiyo.


Kupitishwa kwa bajeti hiyo kunatarajiwa kuimarisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kuboresha huduma za kijamii na kuendeleza miundombinu, hatua ambayo inalenga kuinua ustawi wa wananchi wa Wilaya ya Kishapu katika mwaka wa fedha ujao.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Afisa Serikali za Mitaa Mkuu  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Fabian Kamoga akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani humo cha kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 54.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Februari 12,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson (alievaa shati la draft) akifuatilia kwa makini kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya hiyo cha kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 54.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Februari 12,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Mhandisi Mwandamizi wa Shirika la Umeme TANESCO mkoani Shinyanga Anthony Tarimo akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya hiyo cha kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 54.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Februari 12,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Meneja wa TARURA Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhandisi Elia Mgaya, akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya hiyo cha kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 54.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Februari 12,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Meneja wa Shirika la Umeme TANESCO wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhandisi Hussein Mbulu akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya hiyo cha kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 54.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Februari 12,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Afisa uhusinao na huduma kwa wateja  TANESCO mkoani Shinyanga Emma Nyaki akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya hiyo cha kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 54.3 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Februari 12,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo















0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post