TAMASHA LA AMANI NA MAENDELEO LAENDELEA KUPAMBA MOTO KISHAPU

Na Sumai Salum-Kishapu

Tamasha la Amani na Maendeleo linaloendelea wilayani Kishapu mkoani Shinyanga limeendelea kuvutia mamia ya wananchi huku mashindano mbalimbali ya michezo yakishika kasi na kuonesha ushindani mkubwa.


Mkuu wa Wilaya Atoa Neno la Hamasa

Akizungumza na wachezaji na wananchi waliohudhuria, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter N. Masindi amewapongeza washiriki wote kwa nidhamu, ushindani wa haki na moyo wa kujituma waliouonesha.


“Michezo ni daraja la amani, umoja na maendeleo. Kupitia mashindano haya tunaimarisha afya zetu, tunakuza vipaji vya vijana wetu na tunajenga mshikamano wa kijamii. Nawahimiza vijana kuendelea kujituma, kuwa na nidhamu na kuzingatia sheria za mchezo, kwani michezo inaweza kuwa ajira na chachu ya maendeleo binafsi na ya Taifa.”amesisistiza

 

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki na kushuhudia tamasha hilo hadi siku ya kilele, akisisitiza kuwa amani na utulivu ni msingi muhimu wa maendeleo ya wilaya ya Kishapu na Taifa kwa ujumla.


Tamasha la Amani na Maendeleo limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuibua vipaji, kuimarisha uhusiano wa kijamii na kuhamasisha ari ya maendeleo miongoni mwa wananchi.


Matokeo ya Michezo leo 

🏐 Pete

  • Mwataga 8 vs KSP Sec 1

  • Mwataga 3 vs Watumishi 5

  • Watumishi 6 vs KSP Sec 1

  • Veta 0 vs Isoso Sec 6

  • Veta 3 vs Watumishi Kishapu 13

⚽ Football

  • Bubiki  5       Vs Ukenyenge 0

  • Mwamashele  3  Vs Mwigumbi Combine 1

  • Kishapu Veteran 2 Vs Veta Kishapu 1

🏐 Wavu

  • Watumishi Kishapu 2 Vs Veta Kishapu 0

  • Watumishi Veteran 3 Vs Kishapu Sekondari 0


Mashindano hayo yameonesha kiwango kizuri cha vipaji vya vijana pamoja na kuimarisha mshikamano na urafiki miongoni mwa washiriki.Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter N. Masindi akizungumza na wachezaji na wananchi waliokuwa  kwenye Tamasha la Amani na Maendeleo viwanja vya michezo Shule ya Msingi Buduhe Wilayani humo Februari 26,2026
















































































0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم