DC KISHAPU AZINDUA WIKI YA MISITU KWA KUWEKA MKAZO WA UHIFADHI, MITI 6000 KUBADILISHA TASWILA YA ITILIMA

Na Sumai Salum- Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi amezindua rasmi zoezi la upandaji miti 6,000 katika Kata ya Itilima wilayani humo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani yanayotarajiwa kufikia kilele Machi 21, 2026. 

Uzinduzi huo umefanyika Machi 18,2026 kwa kupanda na kugawa miti ya vivuli na mbao katika shule za msingi pamoja na zahanati za Kata hiyo, huku wananchi wakigawiwa miche mingine  kwa ajili ya kupanda katika maeneo yao ya makazi na mashamba. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Masindi amesisitiza umuhimu wa kupanda na kutunza miti, akieleza kuwa juhudi hizo ni msingi wa kulinda mazingira, vyanzo vya maji na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema kuwa upandaji miti unapaswa kwenda sambamba na utunzaji wake ili kuhakikisha inakua na kuleta tija kwa jamii. Aidha, ametoa wito kwa vijiji kuimarisha na kusimamia sheria ndogondogo zitakazodhibiti uharibifu wa miti hususan unaosababishwa na wafugaji wanaoachia mifugo kula na kuharibu miti iliyopandwa. 

Kwa upande wake, Mhifadhi wa Misitu Wilayani humo, Tumaini Masatu, amesema kuwa TFS inaendelea kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika upandaji miti na kuachana na vitendo vya ukataji miti kiholela. 

Amebainisha kuwa misitu ina mchango mkubwa katika ustawi wa maisha ya wananchi kwa kutoa huduma muhimu kama hewa safi, kuhifadhi vyanzo vya maji na kusaidia shughuli za kiuchumi. Ameongeza kuwa jamii inapaswa kutambua umuhimu wa misitu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, pamoja na kuendelea kuhifadhi misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda bayoanuwai.


Kwa upande wao, wananchi wa Kata ya Itilima wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira pamoja na kugawa miche ya miti bure. Wamesema elimu hiyo imewasaidia kutambua athari za ukataji miti holela na umuhimu wa kupanda na kutunza miti kwa maendeleo endelevu. 

Wananchi hao wameahidi kushiriki kikamilifu katika juhudi za uhifadhi wa mazingira kwa kupanda na kutunza miti, wakieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kulinda mazingira, kuboresha hali ya hewa na kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali za misitu kwa vizazi vijavyo. 


Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ataendelea na zoezi la upandaji na ugawaji miti maeneo mbalimbali ya mijini na Vijijini ndani ya Wilaya hiyo, huku kilele cha maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani kikitarajiwa kuwa Machi 21,2026 yakiambatana na kauli mbiu isemayo "Misitu ni uchumi, tuhifadhi kwa maendeleo ya taifa"
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza wakati wa zoezi wa uzinduaji upandaji na ugawaji miti 6000 ngazi ya Wilaya lililofanyika Kata ya itilima Machi 18,2026 kuelekea siku ya Misitu duniani Machi 21,2026
Mhifadhi wa misitu kutoka wakala wa misitu Tanzania TFS wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Tumaini Masatu akifuatilia kwa makini zoezi la uzinduaji upandaji na ugawaji miti 6000 ngazi ya Wilaya lililofanyika Kata ya itilima Machi 18,2026 kuelekea siku ya Misitu duniani Machi 21,2026 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa mgeni rasmi
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikonokelo Kata ya Itilima wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mholya Yumbu akizungumza kwenye zoezi la uzinduaji upandaji na ugawaji miti 6000 ngazi ya Wilaya lililofanyika Kata ya itilima Machi 18,2026 kuelekea siku ya Misitu duniani Machi 21,2026 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa mgeni rasmi
Kaimu Katibu tawala ambaye pia ni Afisa Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fadhiri Mvanga akizungumza kwenye zoezi la uzinduaji upandaji na ugawaji miti 6000 ngazi ya Wilaya lililofanyika Kata ya itilima Machi 18,2026 kuelekea siku ya Misitu duniani Machi 21,2026 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa mgeni rasmi
Afisa tarafa ya Negezi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Tano Malele akizungumza kwenye zoezi la uzinduaji upandaji na ugawaji miti 6000 ngazi ya Wilaya lililofanyika Kata ya itilima Machi 18,2026 kuelekea siku ya Misitu duniani Machi 21,2026 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa mgeni rasmi
Mratibu wa Mradi kutoka Shirika la Tcrs Mkoani Shinyanga Dkt. Oscar Rutenge
Adam Kilyamale akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya msingi Itilima na Shule ya Msingi Isunda 
Patrick Shija akizungumza kwa niaba ya Vijana
Eva Jackson akizungumza kwa niaba ya wanawake ambao ndio wahanga wa masuara ya mabadiliko tabianchi
Mkazi wa Kijiji cha Ikonokelo Edwin Nyarobi akizungumzia ufaida za zoezi hilo kijijini kwao
Juma Omary Juma akizungumza











































































































































0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم