
Mwenyekiti WA UVCCM Mkoa WA Shinyanga Bernard Werema akizungumza kwenye kikao Cha kamati ya utekelezaji ya UMOJA WA Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoani humo kilichofanyika Machi 13,2026 katika Ukumbi WA Mikutano WA Chama hicho Mkoa
Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 13 Machi 2026 imefanya kikao chake katika Ofisi za UVCCM Mkoa.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Benard Benson Werema, ambapo wajumbe walipata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kimkakati yanayolenga kuimarisha uhai wa Jumuiya na kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za Chama na maendeleo ya Taifa.
Kamati ya Utekelezaji imejadili na kuweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kuimarisha uhamasishaji wa vijana katika ngazi zote za Jumuiya kuendelea kusimamia na kuimarisha nidhamu, mshikamano na uwajibikaji wa viongozi na wanachama, Kujadili maandalizi ya Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa kinachotarajiwa kufanyika Leo, Machi 14, 2026 katika Ukumbi WA Mikutano WA CCM Mkoa.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Benard Benson Werema amesisitiza umuhimu wa umoja, uwajibikaji na ari ya kujituma kwa viongozi na vijana wa Jumuiya, ili kuhakikisha UVCCM inaendelea kuwa nguzo muhimu ya Chama Cha Mapinduzi katika kuwatumikia wananchi na kuimarisha maendeleo ya taifa.














إرسال تعليق