Na Regina Ndumbaro Tunduru-RuvumaMahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela James Hashimu Chingwaru (20), mkazi wa Kijiji cha Mtina, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kujaribu kumbaka bibi mwenye umri wa miaka 75.
Hukumu hiyo imetolewa Machi 16, 2026 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Mhe. Ferdinand Moshi Philip, chini ya kifungu cha 132 (1), (2)(a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 (R.E. 2022).
Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani, mshtakiwa alitenda kosa hilo Disemba 14, 2025 katika kitongoji cha Nyerere, Kijiji cha Mtina wilayani Tunduru, ambapo alikamatwa na baadaye kufikishwa mahakamani Januari 13, 2026 kwa hatua za kisheria.
Mahakama iliridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha shtaka hilo bila kuacha shaka.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Moshi amesisitiza umuhimu wa kulinda makundi yaliyo katika mazingira hatarishi, ikiwemo wazee, dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Aidha, ameeleza kuwa adhabu hiyo inalenga kutoa funzo kwa jamii na kuzuia vitendo vya aina hiyo, huku akiwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kupambana na uhalifu.
إرسال تعليق