MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE YAFANA USHETU, RC MHITA ATOA WITO KUJIKWAMUA KIUCHUMI NA KUJITHAMINI


                      Na Sumai Salum-Ushetu

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amewahimiza wanawake kujitambua, kujiamini na kujithamini ili waweze kutumia kikamilifu fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kuboresha maisha yao na kuchangia maendeleo ya jamii.


Mhe. Mhita ametoa wito huo Machi 8, 2026 alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Kata ya Uyogo, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga.


Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyokwenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka 2026 isemayo “Haki na usawa kwa Wanawake na Wasichana,Msingi jumuishi kufikia dira 2050” Mhita amesema wanawake wana nafasi kubwa katika maendeleo ya familia na taifa, hivyo ni muhimu wakatambua thamani yao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani Mhe. Mboni Mhita akizungumza kwenye sherehe hizo zilizofanyika kimkoa Kata ya Uyogo Wilayani Ushetu mkoani humo Machi 8,2026


Amesema serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia uboreshaji wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 katika halmashauri, inayolenga kuwainua wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi.


“Ni muhimu wanawake mkajiamini na kujitambua thamani yenu. Serikali imeweka fursa nyingi ikiwemo mikopo na programu mbalimbali za uwezeshaji kiuchumi, hivyo zitumieni fursa hizo kujiletea maendeleo na kuboresha maisha ya familia zenu,” alisema Mhita.


Aidha, ameeleza kuwa serikali inaendelea kuimarisha huduma za afya pamoja na mipango mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuongeza ustawi wa wananchi, hususan wanawake ambao ni nguzo muhimu katika familia na jamii.Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Mhe. Frank Nkinda akifuatilia sherehe za siku ya wanawake kimkoa zilizofanyika Kata ya Uyogo Wilayani Ushetu mkoani humo Machi 8, 2026 na Mkuu wa Mkoa Mhe. Mboni Mhita akiwa mgeni rasmi


Katika maadhimisho hayo, Mkuu huyo wa Mkoa pia amekabidhi hati miliki za ardhi kwa baadhi ya wanawake na wanaume, hatua inayolenga kuimarisha umiliki halali wa ardhi na kuwapa wananchi uhakika wa rasilimali hiyo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


Awali akisoma risala ya Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ya kuhusu hali ya mwenendo wa wanawake kiuchumi ngazi ya Mkoa, Katibu wa jukwaa hilo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Khadija Jumanne, amesema serikali imefanya maboresha makubwa katika maisha ya wanawake kupitia utoaji wa mikopo ya 10%, mikopo ya riba ndogo inayotolewa kupitia bank, mafunzo ya ujasiriamali na miradi mbalimbali ya maendeleo inayowahusisha wanawake.


Ameeleza kuwa hatua hizo zimechangia kuongeza ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi, kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla.Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akifuatilia sherehe za siku ya wanawake kimkoa zilizofanyika Kata ya Uyogo Wilayani Ushetu mkoani humo Machi 8, 2026 na Mkuu wa Mkoa Mhe. Mboni Mhita akiwa mgeni rasmi


Katika maadhimisho hayo pia wananchi walipata elimu mbalimbali kutoka kwa wataalamu, ikiwemo elimu ya kujikinga na majanga ya moto, matumizi ya nishati safi, huduma za afya pamoja na uelewa wa umiliki wa ardhi kisheria, kwa lengo la kuongeza uelewa wa jamii na kuwajengea uwezo wa kulinda maisha na mali zao.


Maadhimisho hayo yamewakutanisha viongozi wa serikali, taasisi mbalimbali na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga, ambapo kwa pamoja wameungana kusherehekea mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya jamiiMbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga





































































0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم